Karen ni kitongoji cha Nairobi nchini Kenya, kilichoko kusini magharibi ya katikati mwa jiji. Ni kata ya eneo bunge la Lang'ata, kaunti ya Nairobi.
Inaaminika kwa ujumla kwamba kitongoji kimetajwa kwa jina la Karen Blixen, mwandishi kutoka Denmark wa kitabu cha makala ya kumbukumbu za kikoloni Out of Africa; ambaye shamba lake lilikua kwenye shamba ambako kitongoji hiki sasa kipo. Blixen mwenyewe alikiri katika maandiko yake ya baadaye kuwa "wilaya ya makaazi ya Karen" ili "itwa baada yangu." [1] Naye Remy Martin, muendelezi ambaye alinunua shamba hilo katika mwaka wa 1931 na kuigeuza kuwa eneo la makaazi kwa idadi ya wakaazi wa Nairobi iliyokuwa ikiongezeka kwa haraka, alithibitisha kwamba alikiita kitongoji hicho kwa ajili ya Blixen.
Ukweli wa chanzo cha jina hili ni mgumu kubaini. Blixen mwenyewe alikuwa anajulikana kwa marafiki zake katika Afrika si kama "Karen" lakini kama "Tanne." Shamba lenyewe, lilokuwa shamba la kahawa, lilirasmishwa kama "Kampuni ya Kahawa ya Karen," na ilimilikiwa na familia yake, wengi wao wakiishi Denmark. Mwenyekiti wa bodi alikuwa mjomba wake, Aage Westenholtz. [2] Huenda Westenholtz aliitaja kampuni hii baada ya binti yake mwenyewe, Karen.
Kuna uwezekano kwamba Martin aliita eneo hili jina "Karen" kwa Blixen mwenyewe; huenda hakutambua kwamba jina rasmi la shamba hili lilitokana na Karen tofauti. Hata hivyo - mwaka wa 1975, Martin alithibitisha kwa Judith Thurman, mwandishi wa historia ya Blixen, kwamba kwa kuiita wilaya hii "Karen," alikuwa anafikiria mkaazi maarufu wa shamba hilo.
Kitongoji cha Karen kinapakana na Ngong Road Forest na ni nyumbani kwa Ngong Racecourse. Kinajulikana pia kwa idadi yake kubwa ya Wazungu. Karen na Langata kwa pamoja yanaunda eneo lililojitenga la wakazi wa mapato ya juu.
Nyumbani kwa Blixen bado kumesimama na ni kivutio utalii wa ndani. Nyumbani Orphanage pia iko Karen.